Stori: Musa Mteja,Ijumaa
Wasanii wa filamu Bongo, Jacob Steven na Ester Kiama juzikati walinaswa wakiwa kimahaba gizani, jambo lililoibua maswali mengi.
Tukio hilo lilitokea nje ya Hoteli ya Rodizio iliyopo maeneo ya Masaki jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali walifika kwenye pati ya kumpongeza Mheshimwa Paul Makonda kwa kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar.
Awali, mishale ya saa 6 usiku alionekana Ester akitoka eneo la sherehe kuelekea kwenye ‘parking’ za magari, mara akatokea JB, akamshika mkono (kana kwamba ni mtu na mtu wake) kisha kuelekea kwenye gari.
Paparazi wetu alipoanza zoezi la kuwapiga picha, ndipo Ester alipokimbia na kwenda kumkumbatia JB, jamaa huyo naye akamkingia kifua ambapo mdada huyo alipopata mwanya alitoka nduki kuelekea gizani zaidi huku akivukwa na kiatu chake.
Hata hivyo, baadaye Ester alikirudia kiatu chake na kukivaa ambapo JB alibaki amepigwa butwaa asijue alikotokea paparazi huyo na kuwapiga picha wakiwa katika mazingira hayo.
Akizungumzia tukio hilo, Ester alisema kuwa, hakukuwa na chochote kibaya ila waliongozana na JB kwani ilikuwa ampe lifti kutokana na jamaa huyo kufika kwenye pati hiyo bila gari la
0 comments: