Na Joe Dinga Pefok
WATU watano wamekamatwa
wakituhumiwa kusababisha kifo cha mama mmoja aliyejulikana kwa jina la
Monique Koumate na watoto wake mapacha Jumamosi, iliyopita huko Douala,
Cameroon.
Waliokamatwa ni mkunga wa
hospitali hiyo, wakunga wawili, Mhudumu Mkuu wa chumba cha kuhifadhia
maiti ‘Mortuary’ na mdogo wa marehemu Koumate.
Taarifa za awali zilizotolewa na
mashuhuda wa tukio hilo zinaeleza kuwa, mwanzoni Koumate alifikishwa
hospitali akiwa katika hali mbaya akisaidiwa na mdogo wake aliyejulikana
kwa jina la Agnes. Japo hali ya mama huyo ilikuwa mbaya alikuwa kwenye
hatua za mwisho za kutaka kujifungua, wahudumu wa afya waliokuwa zamu
walikataa kumsaidia kwa sababu hakuwa na pesa kwa ajili ya kulipia
huduma hiyo.
Agnes alijitahidi kuwasihi wahudumu hao
wamsaidie dada yake kwani atawalipa baadaye kwa kuwa hakwenda na pesa
lakini waliendeleza msimamo wao kwamba mpaka alipie kwanza gharama ndipo
watamsaidia kumzalisha.
Kutoakana
na kukoswa msaada, Koumate alifariki muda mfupi baadaye. Baada ya kuona
dada yake ameaga dunia, Agnes aliwaomba tena wahudumu hao wamfanyie
upasuaji marehemu ili kuwaokoa watoto waliokuwa tumboni ilihali
walisikika kucheza, hivyo ikadhihirisha bado ni wazima. lakini wahudumu
wale walisisitiza walipwe kwanza ndipo watoe huduma hiyo. Agnes
alichukua jukumu la kuchana tumbo la marehemu dada yake ili aokoe wale
watoto mapacha.
Agnes alijitahidi akamtoa mtoto wa kwanza akiwa amefariki, wa pili akawa mzima lakini baadaye naye alifariki.
Taarifa zingine kutoka Hospitali
Laquintinie zilieleza kuwa, Koumate alifikishwa hospitalini hapo akiwa
tayari ameshafariki dunia na ndiyo maana mkunga na wahudumu walipuuza
kumpeleka wodi ya wazazi. Wahudumu walieleza kuwa mwili wa marehemu
ulitakiwa kupelekwa mochwarilakini Agnes alisisitiza kuwa, mwili wa
marehemu dada yake lazima ufanyiwe upasuaji ili kutoa wale watoto.
Chanzo kiliendelea kueleza kuwa, Agnes
alipuuzia ushauri wa wahudumuna kuamua kupasua tumbo la marehgemu dada
yake chini ya veranda na kukuta watoto wote wawili wamefariki. Chanzo
hicho kiliendelea kueleza kuwa, Koumate aliyekuwa akiishi Douala V,
mwanzoni alimpelekwa na dada yake kwenye hospitali ya Wialaya ya Nylon
huko Douala III na baadaye alipoona hali imebadilika alimhamishia
Hospitali ya Laquintinie.
0 comments: