Hayo
yalisemwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.)wakati akitoa taarifa ya nchi
katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya
Wanawake Duniani (CSW).
Mhe
Ummy alieleza kuwa Adhma ya Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutoa Elimu bure kwa shule za Msingi
na Sekondari itakuwa na matokeo makubwa ya kuongeza udahili wa wanafunzi
katika Elimu ya msingi, Sekondari na Elimu ya juu.
Akaongeza
kwamba uimarishwaji wa upatikananaji wa elimu kwa wanawake ni msingi
mkubwa wa kuwezesha wanawake kiuchumi, kwakuwa elimu hutoa ujuzi,
maarifa na hali ya kujiamini kwa wanawake kuendea fursa za kiuchumi.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ( Mb)
akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhima ya uwezeshwaji wa
wanawake na uhusiano wake na utekelezaji wa Agenda 2030. katika mchango
wake Waziri anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu wa
Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake amesema Serikali
inatambua umuhimu wa mwanamke katika utekelezaji wa ajenda mpya ya
maendeleo endelevu ( Agenda 2030) na kwamba itaendelea kumwezesha.
Katika
Taarifa hiyo, Mheshimiwa Waziri, alieleza kuwa Serikali ya Tanzania
inatambua kuwa uwezeshaji wa wanawake na Usawa wa jinsia unachangia kwa
kiasi kikubwa kufikiwa kwa wepesi kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (
Sustainable Development Goals). Kwa kutambua hilo Tanzania imejipanga
kuhuisha Ajenda 2030 katika Sera, Sheria na Mipango ya nchi kwa
kuhakikisha kunakuwa wa sheria zinazolenga kuleta Usawa wa Jinsia na
uwezeshaji wa wanawake, ambapo pamoja na mambo mengine utekelezaji wa
Mikakati, Sera na Sheria utaendelea kuzingatia haki ya kielimu kwa
Wanawake na Wasichana.
Mheshimiwa
Ummy, aliongelea pia umuhimu wa Afya kwa wanawake na Wasichana (ikiwa
ni pamoja kupunguza vifo vya wajawazito na watoto) kama njia ya
kumuwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika uzalishaji mali.
Mkutano
huo wa wiki mbili unafanyika NewYork, Marekani kuanzia tarehe 14-24
Machi 2016, ukihusisha wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na
Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubadilishana uzoefu na
kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo Serikali zao zinachukua
katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.
Mheshimiwa
Ummy Mwalimu akiwa pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na Mhe Peter
Serukamba (Mb.), mara baada ya kuwasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu
Masuala ya Maendeleo ya Wanawake.
0 comments: