Tuesday, 29 March 2016

Record label 6 ambazo wasanii wake wanafanya vizuri

Record label ni kampuni inayosimamia wasanii ama brand, kuratibu utengenezaji wa nyimbo, video, usambazaji, masoko, promotion na mambo mengine. Record label pia hutafuta wasanii wapya kwa nia ya kuendeleza vipaji vyao.
page
Nchini Tanzania tumeanza kuona record label mbalimbali ambazo zinafanya vizuri kwa kiasi chake, japo bado hatujafika kule ambako tunatarajia record label zetu zifike. Hapa tumeandaa record label kadhaa ambazo kwa sasa zinafanya poa.
WCB Wasafi
WCB Wasafi ni moja kati ya label kubwa hapa nchini inayomilikiwa na Diamond Platnumz . Label hii mpaka sasa tayari imewatambulisha wasanii 2, Harmonize pamoja na Raymond ambao wote wanafanya vizuri katika soko la muziki hapa nchini. Pia kutokana na kasi yake katika kazi, watanzania wengi wanamatumaini kwamba label hiyo itafanya mambo makubwa zaidi katika siku za usoni.
Rockstar 4000
Rockstar /Sony Music Africa ni kampuni kubwa ya muziki duniani ambayo kwa hapa Tanzania inafanya kazi na Ali Kiba chini ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo nchini, Seven Mosha. Rockstar 4000 ilishirikiana na Ali Kiba ameshatoa kazi, Mwana, Chekecha pamoja Lupela ambapo zote zilifanya poa. Pia mashabiki bado wanataka kuona mambo makubwa zaidi kutoka kwa label hiyo kubwa duniani.

TMK Wanaume Family

Hii ni label Mama iliyochini ya Said Fela ‘Mkubwa Fella’. Label hii imeweza kudumu kwa muda mrefu licha ya kukutana na changamoto mbalimbali zilizopelekea baadhi ya wasanii wake kung’atuka. TMK Wanaume Family kama kundi sasa hivi wanafanya kazi chache za kundi baada ya kudai soko la muziki limebadilika hali ambayo imepelekea Chege Chigunda na Temba kuwa ndiyo wasanii ambao wanafanya vizuri.

Mkubwa na Wanawe

Mkubwa na Wanawe inamilikiwa na Said Fela almaarufu Mkubwa Fela. Label hii inamiliki kundi la Yamoto Band ambao kwa sasa linafanya vizuri pamoja na kundi Salamu TMK ambalo limeanzishwa mwaka 2015 mwishoni. Pia mshindi wa shindano la BSS 2015 Kayumba Juma anasimamiwa na label hii. Pia Mkubwa na Wanawe ina wasanii wachanga zaidi ya 106 ambao wanaandaliwa kuwa mastaa wakubwa wa baadae.

Tip Top Connection

Tip Top ipo chini ya Babu Tale. Mwanzilishi wa label hii ni marehemu Abdul Bonge ambaye ni kaka wa Babu Tale. Kwa sasa label inawamiliki wasanii, Madee Ali, Tunda Man, Dogo Janja ambao wote wanafanya vizuri kimuziki. Pia Tip Top ni moja kati ya label kubwa kutokana wasanii wake kukaa kwenye game kwa muda mrefu bila kutetereka.
QS Mhonda
Hii ni label mpya ambayo imeanzishwa miaka ya karibuni na QSJ Mhonda. Label hii pamoja na uchanga wake tayari imefanikiwa kuwarudisha msanii Q Chief pamoja na MB Dog ambao walipotea katika muziki. Pia hivi karibuni label hii ilitangaza kumsign mwimbaji Bushoke ili aongeze nguvu katika bendi ya ‘QS International Band’. Pia label hii inamiliki wasanii wengine wachanga kwa lengo la kuendeleza vipaji vipya.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: