Tuesday, 29 March 2016

Uongozi wa Bagamoyo Sober House wazungumzia maendeleo ya Chidi Benz


Ikiwa ni wiki moja toka Chidi Benz achukuliwe na meneja wa Diamond, Babutale pamoja Kalapina na kupelekwa Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa Sober hiyo umeeleza maendeleo ya rapa huyo.
Babu Tale, Chidi Benz na Kalapina
Akizungumza katika kipindi 360 cha Clouds TV Jumanne hii, Mkurugenzi wa Life and Hope Rehabilitation Organization, Bwana Al-Karim Banji amesema Chidi Benz amekuwa msikivu na afya yake imeanza kurudi.
“Chidi Benz anaendelea vizuri sana, tena nimeshangaa amepata hamu ya kula kitu ambacho ni tofauti kwa waathirika wengine,” alisema Bwana Banji.
“Mimi mwenyewe nilikaa na Chidi Benz nikaongea nae na alinisikiliza sana, nilimwambia maneno mengi ya busara, alinisikiliza na akaniambia mimi niko tayari kubadilika. Kwa hiyo Chidi Benz anaendelea vizuri na ana kula vizuri yaani yupo very positive,” aliongeza.
Banji alisema ndani ya miezi miwili mpaka mitatu Chidi Benz anaweza kukaa sawa kabisa kwa kuwa anapitia semina mbalimbali za kumjenga kiakili.
Pia Banji amewataka watanzania kuacha kumsema vibaya kwa ile ni hatua ya maisha ambayo binadamu yeyote anaweza kuipitia.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: