Sunday, 13 March 2016

TAHADHARI;Jennifer Mgendi wa Facebook ni 'FEKI'



Ndugu watanzania na wote wanaofuatilia kazi zangu nasikitika kuwajulisha kuwa kuna Jennifer Mgendi feki kaibuka Facebook kafungua akaunti kwa jina langu kachukua na picha zangu ambazo zinapatikana mtandaoni kaziweka kwenye akaunti yake ili kuwaaminisha watu kuwa ni Jennifer Mgendi.

Mtu huyu ambaye naamini hana lengo lingine zaidi ya kunichafua amekuwa akipost vitu anavyojua mwenyewe na kuwasiliana na watu mbalimbali ambao baadhi wamekuwa wakinipigia kufuatilia mambo ''tuliyoongea facebook''!! 

Cha ajabu amekuwa akiwapa namba yangu ya simu ambayo ipo kwenye cd zangu ili kufanya watu wazidi kuamini kuwa wanachat na Mimi.

Napenda kuujulisha umma kuwa sipo Facebook wala sichat na mtu yoyote Facebook. Mawasiliano ninayotumia ni ya simu ya mkononi na email kama zinavyoonekana kwenye dvd zangu.

Kwa ujumbe huu natoa onyo kwa mtu huyo kuacha mara moja kwani mamlaka husika inalifanyia kazi jambo hili na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: