April 21 Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
amezungumzia kuhusu habari zilizokuwa zinaongelewa kuwa anakosea
kutumbua majipu hadharani, habari hizo zimekuja siku chache baada ya
Rais Magufuli kutangaza hadhari kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe.
“Wapo
wengine wanalalamika wanasema tunawanyanyasa sio haki za binadamu kwa
sababu tunawatangaza hadharani, kwa hiyo wao walikuwa wana haki ya
kuwaibia hadharani watanzania, waliwaibia watanzania hadharani na lazima
tuwatangaze hadharani, mateso waliowapa watanzania mamilioni kwa
kuwaibia wacha na wao wayapate” >>> Rais Magufuli
0 comments: