Thursday, 21 April 2016

Msanii huyu mchanga adai ana ndoto ya kuja kumuoa Vanessa Mdee



Wanasema ota ndoto kubwa. Kwa Bright ndoto yake ni kuja kumuoa Vanessa Mdee.
IMG-20160418-WA0010
Bright (katikati)
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio jana wakati akitambulisha wimbo wake mpya ‘Nitunzie’ aliomshirikisha Barakah Da Prince, Bright ambaye jina lake halisi ni Rashid Said alisema kuwa hajali kuwa Vee Money yupo na Jux kwa sasa.
12930981_546673255505145_22001411_n
Kauli ya Bright iligeuka kuwa ‘komedi’ kwa watangazaji wa show hiyo. “Hapana msicheke kwasababu ni kitu ambacho naongea nipo serious kabisa,” alisema Bright.
“Nataka kumuoa, Vee Money ni mwanamke mzuri kwanza, ni mwanamke mwenye mvuto ambao mwanaume yeyote aliye kamili lazima avutiwe naye.”
Bright amesema anajipanga kutupa ndoano yake kumnasa mrembo huyu. “Hata kama Jux yuko naye, hawajaoana wale, kwahiyo mimi nina nafasi pia ya kuweza kumuambia,” alisisitiza.
Jux watch out, you got competition. Usikilize wimbo wa Bright hapo chini.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: