April 21, 2016 chama
cha ACT – Wazalendo kilifanya mkutano mbele ya waandishi wa habari na
kuzungumza kuhusu kung’atuka kwa Katibu Mkuu wao aitwae Samson Mwigamba ambaye anatarajia kwenda Kenya kimasomo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho Mama Anna Elisha Mghwira alisema..>>>‘Katibu mkuu wa chama cha ACT –Wazalendo
ndugu Samson Mwigamba ataanza masomo ya Shahada ya Uzamili ya Biashara
(MBA) katika chuo Kikuu cha Kenyatta kuanzia mwezi Mei 2016 kufuatia
hatua hii ameomba aruhusiwe kung’atuka nafasi yake ya katibu Mkuu wa
chama’– Anna Elisha Mghwira
‘Kufuatia
hatua ya kung’atuka kwa katibu Mkuu, kamati ya Uongozi imeiagiza kamati
ya Chama ya Mafunzo na Uchaguzi ianze mchakato wa kumpata katibu Mkuu
mpya kwa kuzingatia katiba na kanuni za uchaguzi wa chama‘ – Anna Elisha Mghwira
0 comments: