Miongoni mwa habari kubwa za dunia hivi karibuni ni Nyaraka za Panama ‘Panama Papers‘
zilizofichua kashfa ya ukwepaji kodi na utakatishaji fedha ulikofanywa
na viongozi wa mataifa mbalimbambali, watu maarufu na wanasiasa ambapo
baada ya nyaraka hizo kuzidi kuwaumbua watu wakubwa duniani, Tanzania
Takukuru wakasema itacheck kama kuna watanzania wamo kwenye list hiyo.
Inasemekana nyaraka hizo za Panama zilizovuja pia zilimtaja kiongozi na mwanzilishi wa kanisa Synagogue Church of All Nations ‘SCOAN’, T.B Joshua na mkewe Evelyn kwamba wanamiliki kampuni ya Chillon Consultancy Limited.
Tuhuma
hizo zilianza kuchapishwa na mtandao wa habari wa Premium Times ambapo
kupitia official page yake ya facebook T.B Joshua ameonya dhidi ya kauli
za kumkashifu yeye na kanisa lake na kusisitiza kwamba yeye sio
mfanyabiashara na hana hizo biashara.
TB Joshua amesema habari hizi
zimeandikwa na Mwandishi wa habari ambaye wamekua hawaelewani toka jengo
la kanisa hilo lianguke na kupoteza maisha ya watu, kutokana na
kutoelewana huko TB Joshua amekua akipokea mfululizo wa habari mbaya
zinazoandikwa na Mwandishi huyo wa habari.
0 comments: