Jeshi
la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa Majambazi
watatu yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa jina la
Emmanuel Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo yalianza
kujibizana risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha polisi na
kufika katika eneo la tukio.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita Kawawa, amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Akizungumza
kwa njia ya simu kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP
Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi punde wanapoona dalili
zozote za kiuhalifu zinafanyika.
Katika
tukio hilo jeshi polisi limefanikiwa kukamata bunduki mbili moja aina
ya Short Gun na moja ya kivita aina ya Uzgun, bomu la kutupa kwa mkono,
kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na magazine mbili za
bunduki.
0 comments: