KUFUATIA
mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu
wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa
kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka
wahusika wote kujisalimisha.
Katika
hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa
Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi
wa kisiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha
wafuasi wao wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.
Kauli
hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa
habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi
yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga
marufuku mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata
ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye
mkono wa sheria.
"Kwasababu hiyo basi,kwa
hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na
kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini
linapiga marufuku mikutano yote ya ndani" amesema.
Amesema Jeshi hilo limebaini
kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kuchochea wananchi na
kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi la
polisi
Aidha
CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati
wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G
9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa
aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa
Mbande.
"Katika
tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora
silaha mbili aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki
hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na
kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.
Alisema
katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu
waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la
polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa
kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema
endapo watapigwa na polisi Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
0 comments: