August
23 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka Mabalozi wanne
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi
hao ni Roberto Mengoni -Balozi wa Italia hapa nchini, Kim Yong Su –
Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini, Mohamed
Hassan Abdi – Balozi wa Jamhuri ya Somalia hapa nchini na Paul Sherlock –
Balozi wa Ireland hapa nchini.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati za utambulisho za Mabalozi
hao Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha
nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itawapa ushirikiano wa kutosha ili kuendeleza na kuuimarisha zaidi uhusiano ulipo kati ya nchi hizo na Tanzania.
Dkt.
Magufuli amewaambia Mabalozi hao kuwa katika kipindi cha kuanzia Mwaka
2016/2017 hadi 2020/2021 Tanzania imedhamiria kutekeleza mpango wa
ujenzi wa viwanda, hivyo amezialika nchi zao na sekta binafsi katika
nchi hizo kuungana na Tanzania katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda
na biashara.
Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ireland Paul Sherlock alisema…….>>>“Naomba
kukuhakikishia kuwa Wafanyabiashara watakaokuja kuwekeza ama kufanya
biashara, mitaji yao itakuwa salama na Serikali yangu itatoa ushirikiano
wa kutosha kuhakikisha uwekezaji huo unafanikiwa na unanufaisha pande
zote mbili”
Rais Magufuli na balozi wa Italy hapa nchini Roberto Mengoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli na Roberto Mengoni mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
.
Rais
Magufuli na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa
nchini Kim Yong Su mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho
.
.
Rais
Magufuli na Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi mara
baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za
Utambulisho.
Rais Magufuli na Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock Ikulu jijini Dar es Salaam.
0 comments: