Thursday, 22 May 2014

BIFU JIPYA KATI YA WEMA, STEVE NYERERE NA MTITU. NUSURA WAZICHAPE KWENYE MSIBA WA KUAMBIANA.


Na Mwandishi wa Xdeejayz Tanzania
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wasanii Wema Sepetu na Mtitu usiku wa kuamkia jumatatu walizinguana kinoma kaisi cha kutaka kutoana roho kwa kile kinachodaiwa Wema kujibu nyodo mara baada ya kupata taarifa za msiba wa Adam Kuambiana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo eneo la tuki kilisema kuwa chanzo cha ugomvi huo ni baada ya kifo cha Adamu wasanii wote walifika kwa wakati eneo la msiba isipokuwa Wema Sepetu ambae hakuonekana mapema.
Hata hivyo baada ya kutoonekana Wema msibani mwenyekiti wa Bongo Movie alimpigia simu Wema na kumueleza kama ameusikia msiba wa Adamu" Unaambiwa Wema alimjibu kunya steve kiasi cha kukata simu, kwani alimwambia kama ndiyo ameusikia msiba kwa hiyo steve anatakaje?" Kilisema chacho hicho
Hata hivyo Wema inadaiwa aliendelea kusema kama Adamu amekufa si siku zake zilikuwa zimefika, ndipo steve alipomwambia anatakiwa aonekane msibani kwani wasanii wenzake wote wapo yeye tu ndo haonekani, ndipo Wema alipojibu kuwa mbona yeye alipofiwa na babaake hakumuona Adamu kwa hiyo asilazimishwe kama ataenda basi kwa hiari yake. Duh.
Hata hivyo Xdeejayz ilimtafuta Wema kupitia simu yake ya kiganjani ili kuelezea tukio hilo lakini hakuweza kupatikana hadi habari hii inawafikia wasomaji wetu.
Hata hivyo siku ya Jumatatu usiku wakati wa mkesha ndipo Wema alipoonekana akiwa na Aunt Ezekiel ambapo mtitu ambae alikuwa bwax huko msibani Bunju na alipomuona Wema akaanza kumtusi ya nguoni ndipo wakaanza kujibizana kiasi cha kukunjana huku akimpaka juu ya majibu aliyoyatoa kwa mwenyekiti huyo wa bongo movie.
Hata hivyo hadi chanzo cha xdeejayz  kinaondoka eneo la tukio kiliacha mtiti mzito ukiendelea.
SOURCE: XDEEJAYZ TANZANIA
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: