Wednesday, 21 May 2014

Kampuni tano zinawania leseni za gesi na mafuta Tanzania


Tanzania gas rig
Ilitarajiwa kampuni nyingi zaidi zingewania leseni hizo kuwekeza mabilioni ya dola, lakini tano kati ya nane zimewasilisha maombi.
Kampuni tano zimepanda dau la kutaka kununua leseni za kutafuta mafuta na gesi katika himaya ya Tanzania.
Hata hivyo idadi hiyo ni ndogo zaidi kuliko vitalu vinane vilivyokuwa vikinadiwa katika duru hii, TPDC imeeleza.
Tanzania, ambayo imegundua kiasi kikubwa cha gesi ya asili katika mikoa ya kusini, ilitangaza vitalu saba vya maji marefu baharini na kimoja katika Ziwa Tanganyika.
Kampuni ya CNOOC Ltd na Gazprom inayoendeshwa na serikali ya Urusi ni miongoni mwa makampuni makubwa ya kigeni yaliyowasilisha maombi yao katika mzunguko huo wa nne.
Miamba mingine ya nishati Statoil na ExxonMobil, ambayo imegundua kiasi kikubwa cha gesi Tanzania, iliwasilisha maombi ya pamoja kupata kitalu kimoja.
“Mchakato wa kutathmini utaanza mara moja na tutatangaza washindi wa mnada haraka iwezekanavyo kadri muundo wa ushughulikiaji wa leseni unavyoruhusu,” Yona Killagane, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) aliieleza Reuters.
Killagane hakusema lini washindi watatangazwa. Muda wa mwisho kuwasilisha maombi ilikuwa Mei 15.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: