Haina ubishi kua Diamond na Wema ndio wasanii pekee wanaoongoza kwa kuandikwa na magazeti na mtandaoni. Wote wawili wanakubalika sana ukianza na Diamond katika mziki na Wema katika Bongo Movie. Usisahau kua Diamond nae kaingia katika Bongo Movie na kaigiza na Wema movie ambayo hadi leo bado inasubiriwa kwa hamu kubwa. Lol.
UNAWEZA SOMA : STAA WA KIKE BONGO ATUPIA MTANDAONI PICHA YA UTATA..JE WAWEZA MTAMBUA NI NANI?
Kama utakua ni mpenzi wa Instagram naamini utakua umewafollow Wema na Diamond kwani ndo watu wanaongoza kwa kuongelewa sana Insta na pia ndio wenye followers wengi zaidi kuliko watanzania wengine wote waliopo katika Instagram. Mpaka Tunaandika habari hii Diamond alikua na followers 120,563 na Wema akmfatia akiwa na Followers 111,450.
Unaweza ukaona ajabu kuhusu hili kani ukweli ni kwamba pamoja na kua Diamond na Wema ni wapenzi lakini hakuna aliyemfollow mwenzake kwenye Instagram. Nahisi kila mtu kauchuna akisubiria mwenzake aanze kumfollow.
UNAWEZA SOMA : Hahaha Lulu..!! Baada Ya Diamond Kuchaguliwa Kuwania Tuzo Za BET, Hiki Ndicho Kituko Alichoandika Lulu Na Kumuagiza Diamond..!!
0 comments: