Skyner Ally |
Habari za awali zilisema kuwa, ndoa ya Skyner iliingia mdudu baada ya
mumewe kugundua kuwa alinunua ‘mbuzi kwenye gunia’, kwani bidada huyo
alikuwa na ujauzito wa mtu mwingine.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.
Hata hivyo, minong’ono ilikuwa inasema kuwa, mimba hiyo ilikuwa ya Nay ingawa awali, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua kuhusiana na ishu hiyo.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa Oktoba 7, 2011 nyumbani kwa dada yake,
Magomeni – Mapipa, Dar es salaam na kufika tamati kabla ya mwezi
Novemba, dah!
Ripoti zinaonesha kuwa, baada ya Skaina kutemwa na Saad alimweleza Nay
sababu na kutimkia kwao Iringa ambapo alipojifungua alimweleza ukweli
mwenzi wake huyo kuhusu ujio wa mtoto wao.
Wawili hao wameelezwa kuwa na mawasiliano ya karibu lakini ya siri kwa
muda mrefu ila hivi karibuni, wote waliamua kuutua mzigo huo na kuweka
mambo hadharani ambapo kwa upande wa Skyner alisema: “Nadhani mmechelewa
tu kujua, lakini habari ndiyo hiyo.”
Nay alipoulizwa, alijibu kwa kifupi sana: “Ni kweli lakini ni mambo ambayo huwa sipendi kuyazungumzia sana.”
Skyner |
Ili kuthibitisha ukweli huo, wikiendi iliyopita, baada ya Nay kutwaa
tuzo moja ya Kili katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana,
Skyner alitupia maneno ya kumpongeza Nay katika ukurasa wake kwenye
Mtandao wa Kijamii wa Instagram yaliyosema:
“Hongera baba mtoto wangu kwa kuchukua tuzo, Mungu akuzidishie baraka na
maisha marefu ili mwakani uweze kuchukua tuzo nyingi zaidi. Navutiwa
sana na kazi zako dady wetu (akimaanisha yeye na mwanaye).”
0 comments: