|
Coletha |
Star wa muda mrefu katika tasnia ya filamu Swahiliwood Coletha Raymond
amewapa makavu live wasanii na wanawake wanaopenda kujichubua kwa kusema
kuwa hawajitambui ndiyo maana wanadhani kuwa mweusi si urembo na weupe
ndiyo urembo. Coletha alisema kuwa wengi wanaotumia mkorogo huishia
kuharibu ngozi zao kuliko walivyokuwa awali. Coletha alisema kuwa wapo
wanawake wengi weusi ni wazuri na warembo sana kuliko wanawake weupe kwa
hiyo wanaojichubua na kutumia mkorogo wakaulize kwanza madaktari
madhara ya kujichubua ambayo mojawapo ni kupata kansa ya ngozi.
0 comments: