Muongozaji wa video za muziki Tanzania, Adam Juma wa Next Level anatamani kumtengeneza msanii mwingine mpya atakayefata nyayo kama za Diamond kimafanikio.
Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds Fm, AJ amesema ndoto yake kwasasa ni kuona anamsimamisha msanii mpya mwenye nyimbo nzuri.
“Natamani kupata ngoma kali, natamani mtu aimbe nyimbo nzuri haijalishi ni msanii gani, sina wigo wa kusema nifanye kazi na msanii flani mkubwa sina msanii mkubwa sina msanii mdogo, naamini saizi nachotaka kufanya kuna mtu ameshatuonesha moyo Diamond alipofikia, the whole entire of Afrika wanamtaka, nataka kumtengeneza mwingine, nataka kumtengeneza mwingine kutoka chini kabisa asimame, kwasababu bado nina ndoto, bado nina vitu kichwani kwahiyo msanii yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi anaweza kufanya kazi na mimi.”– Adam Juma
0 comments: