Nimeipata hii takwimu ambayo sikuwa nafahamu, kumbe Facebook ina watumiaji Milioni 120 wa Mtandao huo ndani ya Africa pekeyake !!
Story nyingine kuhusu Facebook
kwa sasa hivi ni ishu ya kusogeza Office zao mpaka ndani ya Jiji la
Johannesburg Afrika Kusini na tayari hapo ndio yatakuwa Makao Makuu ya
shughuli zao zote zinazohusu Facebook Afrika, Nunu Ntshingila ndio Boss ambaye kachukua ajira kusimamia Kampuni hiyo.
Kingine ni kwamba jamaa wameamua kuisogeza Facebook
ndani ya Afrika kama njia ya kusogea karibu ya wateja wao wengi ambao
ni Wafanyabiashara wanaotumia Mtandao huo katika kutangaza biashara zao.
Facebook
iliangalia siku nyingi sana jinsi ya kuingia kwenye soko la Afrika,
waliwahi kurahisisha huduma kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuweka App
maalum ambayo mtumiaji hakatwi pesa wala hatumii data kwenye
kuchat, mpango wao mwingine ni kuhakikisha wanamfikia kila mtu hata
ambae hana uwezo wa kumiliki simu yenye uwezo wa Internet.
Mpango walionao kwa sasa ni kuajiri wafanyakazi 25 ili ofisi ya Johannesburg ijitosheleze na kazi iendelee kama kawaida.
0 comments: