Kumekuwepo na matukio ya baadhi ya
wazazi kuwanyanyasa na hata wengine kuripotiwa kuwaua watoto wao wa
kuwazaa wenyewe kutokana na sababu mbalimbali.
Headlines nyingine leo zinatokea kule
India ambapo mama mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya kuripotiwa kumla
mtoto wake wa miaka minne huku akiwa hai.
Pramila Mondal ambaye
anadaiwa kuwa na matatizo ya akili alifanya kitendo hicho akiwa
nyumbani kwake na kukutwa na shemeji yake akiendelea kumla mtoto huyo
sehemu mbalimbali za mwili wa mtoto wake huyo ambaye alikuwa wa kike.
Baada ya Polisi kufika na kumshilika mama huyo, mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya Malda Medical center huku akiwekwa katika chumba cha uangalizi maalum kutokana na kuwa na majeraha makubwa.
Polisi walisema pamoja na mama huyo
kudaiwa kuwa na matatizo ya akili pia pombe pamoja na madawa vimechangia
yeye kufanya tukio hilo.
0 comments: