Ndani ya wiki moja baada ya Serikali ya
Marekani kupitisha Sheria ya kuruhusu Ndoa za jinsia moja kwa raia wake
kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusiana na maamuzi
hayo.
Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.
Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe
alisema hawezi kupingana na maamuzi ya nchi hiyo kwani ni sheria ambayo
imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda
mpaka Washington kuomba kufunga ndoa na Rais Barack Obama.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Marekani
imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni wafuasi wa shetani wanaoitukana
taifa la Marekani akisisitiza Marekani imechafuka na wanaiendesha nchi
kwa dhana zao binafsi ambazo ni potofu.
0 comments: