Muigizaji wa filamu, Aunty Ezekiel ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto wa kike, amedai kuwa licha ya kuzaa nje ya ndoa, bado anaamini ndoa yake ipo pale pale.
Aunty akiwa na mpenzi wake Mose Iyobo
Akizungumza na Bongo5 leo, Aunty aka Mama Cookie, amesema aliamua kuzaa na Moses Iyobo, dancer wa Diamond Platnumz kwakuwa muda wa kuwa mama ulikuwa umefika.
“Mimi niliamua kupata mtoto baada ya kuona wakati umefika,” amesema.
“Kwasababu siku zinaenda pamoja na umri inabidi maisha yaendelee mbele. Ndoa yangu ipo kama ilivyokuwa mwanzo, haijavunjika, sijawahi kuongea kama nimezaa nje ya ndoa au ndani ya ndoa lakini mwisho wa siku ndoa yangu bado ipo,” ameongeza.
“Haya ni maisha na vitu vinavyozungumzwa vipo kama vilivyo, lakini familia yangu na watu wa karibu wanaelewa nini kinaendelea ndani yake na watu niliokuwa nao wanaelewa na sidhani kama itakuwa right kuongea kwenye media. Lakini watu wajue baba yake ni Mose,” amesisitiza muigizaji huyo.
Aunty Ezekiel akiwa na mtoto wake Cookie
Pia Aunty amewatoa hofu mashabiki wa kazi zake kwa kusema kuzaa kwake sio mwisho wa kuigiza.
“Kupata mtoto kwenye maisha yangu ni kitu kizuri kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo nimepunguza na nimekuwa mama mwenye majukumu, ninapofanya vitu vyangu najua kesho na kesho kutwa kuna mtu ananitegemea. Pia kuzaa kwangu sioo kwamba kutaua sanaa yangu, sanaa yangu ipo pale pale na hata nitakapomaliza kulea nitakuwa na vitu vingi zaidi kwa sababu natumia muda mwingi kulea Kwahiyo nikirudi wategemee vitu vikubwa zaidi ingawa kuna kazi ambazo niliziandaa zitatoka wakati ninalea.”
0 comments: