Msanii Harmonize kutoka WCB, amesema kamwe haamini kama kujihusisha na uchawi pamoja na ushirikina kunaweza kumsaidia msanii kutusua kimuziki.
Aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye
kipindi kimoja cha Tv msanii huyo amesema kuwa yeye anaamini Mungu na
kipaji ndivyo vinaweza kumfanya mtu ang’are kisanii.
“Siamini kuwa uchawi
una nafasi kubwa kwenye muziki,ingekuwa hivyo basi watoto wa waganga
ndio wangekuwa wana hit peke yao,Mungu ndio kitu pekee cha kuamini
pamoja na talent yako”
0 comments: