Madee afunguka kuhusu Raymond kwa mara ya kwanza tangu aachie wimbo wake wa ‘Kwetu’ chini ya WCB.
Madee ambaye ndiye alimuunganisha Raymond kwenye kundi la Tip Top Connection kabla ya kujiunga na lebo ya WCB.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio,
Madee amesema, ‘ninachokiona nilikitarajia kwamba Raymond atakuwa mtu
fulani’.
“Raymond yuko vizuri anafanya vizuri ni mtu ambaye nimekaa naye najua
uwezo wake, ninachokiona nilikitarajia kwamba Raymond atakuwa mtu
fulani, Raymond ana kila kitu ambacho msanii anatakiwa awe nacho, mara
nyingi huwa naenda nae studio,” aliongezea Madee.
Madee kwa sasa ameachia nyimbo yake ‘Migulu Pande’ ambayo imeanza
kufanya vizuri kwenye media mbalimbali japo haina muda mrefu tangu
aitoe.
0 comments: